Samatta amepewa jezji yenye namba 77 mgongoni
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mchezaji bora wa ndani wa
Afrika Mbwana Samatta leo ametambulishwa rasmi na ameshakabidhiwa jezi
na klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuanza majumu mapya ya
kutupia wavuni akiwa na klabu hiyo. Mbwana Samatta akitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Genk, Samatta amesaini mkataba unaomalizika msimu wa mwaka 2019-2020.
Samatta amejiunga na Genk akitokea TP Mazembe ambapo alicheza kwa
miaka mitano (5) tangu mwaka 2011 alipojiunga na klabu hiyo akitokea
klabu ya Simba SC hadi mwaka 2015. Samatta akiwa kwenye press conference akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga na klabu ya Genk
Mkataba wa Samatta na Mazembe ulikuwa unamalizika mwezi April mwaka
huu lakini tayari amesaini mkaba mpya na klabu hiyo ya barani Ulaya. Samatta kwenye picha ya pamoja na moja ya viongozi wa Genk
Angalia picha zaidi za Samatta wakati akitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari. Samatta kwenye picha ya pamoja na moja ya viongozi wa GenkViongozi wa klabu ya Genk wakimkabidhi Samatta jezi ya klabu hiyo tayari kwa majukumu mapyaSamatta akiwa kwenye press conference akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo Picha ya X-ray inayoonesha mguu wa kushoto wa Samatta wakati akifanyiwa vipimo na kufanikiwa kufaulu vizuri