Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Wednesday, 16 September 2015

DJ Fetty anatangaza kuacha kazi ya utangazaji…

Jina lake ni Fatma Hassan aka DJ Fetty, moja ya Watangazaji ambao wamepata majina makubwa sana TZ na East Africa kutokana na kazi ya Utangazaji ambapo ana mchango mkubwa pia kwenye muziki wa Bongo Fleva kama Mtangazaji wa show ya Entertainment,XXL ya Clouds FM.IMG-20150915-WA0006September 15 2015 Show ya XXL inaandika Historia nyingine tofauti ambapo DJ Fettyametangaza kuacha kazi ya Utangazaji na kuingiza nguvu yake zaidi kwenye masuala ya Biashara… wakati Fetty anatangaza hivyo, presenter mwingine pia Kened the Remedyameungana na Timu ya XXL kwa mara ya kwanza.IMG-20150915-WA0002IMG-20150915-WA0007-1UGANDAN-YOUNG-MAN-WITH-OLD-WIFE
Ndani ya Studio ya Clouds FM, hapo yuko KenneddAdam MchomvuDJ ZeroB Dozen na DJ Fetty.

MATOKEO YA LIGU KUU VODACOM TIMU ZILIZO CHEZA JANA

VPL logo
Mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara zimeendelea leo kwenye viwanja saba huku timu 14 zikipambana viwanjani kuwania pointi tatu muhimu kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo msimu huu.
Jijini Tanga wenyeji Mgambo JKT walikuwa wakiwaalika ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba kwenye uwanja wa Mkwakwani ambapo Simba wamechomoza na ushindi wa goli 2-0 magoli yaliyofungwa na Justice Majabvi na Hamisi Kiiza.
Timu ya Majimaji ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea imechomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, pambano jingine lilikuwa ni kati ya Toto Africans ‘wana kishamapanda’ ambao wao walikuwa nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mtibwa Sugar mchezo uliomalizika kwa Mtibwa kutwaa pointi tatu kwa kuifunga Toto goli 2-0.
Kwenye dimba la Sokoine, timu ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya maafande wa JKT Ruvu. Azam wakiwa ugenini kwenye uwanja wa CCM Kambarage wamefanikiwa kuitungua Stand United kwa goli 2-0 wakati Ndanda FC wakiwa nyumbani kwenye dimba la Nangwanda Sijaona wameandika ushindi wa kwanza wakiichapa Coastal Union kwa goli 1-0.

Lissu amtaja JK kuhusika Richmond

TATIZO LA UMEME KUISHA LEO


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.

Aidha, kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na  inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin, alisema kazi ya kuwasha mitambo hiyo inahitaji umakini mkubwa  kutokana na mfumo unaotumika kuwa mpya.

Alisema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi imekamilika na tatizo lililokuwapo la kukatika umeme lilitokana na matengenezo ya mfumo mpya yaliyokuwa yakiendelea kwa ajili ya kuwashwa kwa mitambo hiyo mipya.

Aliwataka wananchi wawe na subira wakati kazi hiyo ikiendelea na hadi kufikia leo itakuwa imekamilika na umeme utapatikana kwa uhakika baada ya kuanza kuzalishwa kwa kutumia gesi kutoka Mtwara.

 “Kuanzia leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:

“Watanzania wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya Mtwara kwani  kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”

Severin alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150).

Alisema mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo.

Severine alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha

@@Download Ze Bato ft Baraka da price_Niacheni

NYENGINE TENA KUTOKA KWA ZE BATO SAFARI HII KAMSHIRIKISHA MSHINDI WA TUZO YA MSANII BORA WA KIUME CHIPUKIZI BARAKA DA PRICE
kudownload nyimbo hii ze bato ft baraka da price bonyeza link 
https://www.hulkshare.com/5qnhrg35bcsg

Monday, 7 September 2015

HOTUBA YA MGOMBEA EDWARD LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU

Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
  1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
  2. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
    • Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
    • Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
    • Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
    • Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
  3. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
  4. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
  5. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
  6. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
  7. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
  8. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
  9. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
  10. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
  11. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
  12. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.Ndugu watanzania
  13. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
  14. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
  15. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
  16. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
    • Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
    • Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
    • Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
    • Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
    • Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
  17. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
  1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
  2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
  3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
  4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
  5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
  6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
  7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata
AFYA
  1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
  2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
  3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
  4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
  5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
  6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
  1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
  2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
  3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
  4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
  5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
  6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
  7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
  8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
  9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
  10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
  11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
  1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
  2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
  3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
  4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
  5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
  6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania
VIWANDA
  1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
  2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
  3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
  4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda
UCHUMI
  1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
  2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
  3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
  4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
  5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
  6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga nyumba bora
  7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
  1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
  2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
  3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
  1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati
  2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.
  3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
  4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
  5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
  6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
  7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.
  8. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
  9. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
  1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
  2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
  3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
  4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
  1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
  2. Tutaboresha miundobinu ya sheria na kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
  3. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
  4. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
  5. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
  1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
  2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
  3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
  4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
  5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
  6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
  7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
  1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
  2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
  3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
  4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
  5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
  6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
  1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
  1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
  2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
  3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
  4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
  5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
  1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
  2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
  3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
  4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
  5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
  6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
    7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
  1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.
  2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
  3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
  4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
  1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
  2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
  3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
  4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
  5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.
  6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
  7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana

SABABU 10 KWANINI JOHN MAGUFULI ATASHINDA UCHAGUZI MKUU WA URAISI 2015




Tanzania bara na visiwani yako majimbo ya uchaguzi 266, CCM imesimamisha wagombea Ubunge katika majimbo yote 266 huku Chadema na washirika wake wa Ukawa wakiwa wamesimamisha wagombea katika majimbo 211 (138 toka Chadema). Kati ya majimbo hayo 266, CCM tayari imepita bila kupingwa majimbo 7.

Ukichukua majimbo 259 yaliyobaki na kutoa 211 ambayo Chadema na washirika wake wamesimamisha wagombea unabaki na majimbo 48 ambayo CCM haina upinzani wa Chadema wala washirika wake wa Ukawa. Majimbo haya 48 CCM ina uhakika wa kushinda walau kwa asilimia 90, ushindi huu si kwa Wabunge tu bali pia kwa mgombea Urais wa CCM.

Watanzania waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2015 ni milioni 24.2. Takwimu zinaonyesha CCM ina wanachama hai wapatao milioni 8 wenye kadi na wanaolipia ada zao za uanachama kila mwaka. Kuondoka kwa Edward Lowassa katika Chama Cha Mapinduzi kunamaanisha Magufuli hatapata kura zote milioni 8 za wana CCM na pia kihesabu si rahisi wana CCM wote milioni 8 kujitokeza siku ya kupiga kura.

Utafiti unaonyesha kwamba wana CCM watakaopiga kura hawatazidi asilimia 90 ya wanachama wake (milioni 7.2) huku milioni 7 kati yao wakimpigia kura John Magufuli. Historia ya CCM inaonyesha ni wanachama wachache sana humpigia kura kada mwenzao anapohama kugombea nafasi kwa chama kingine, hasa nafasi ya Urais (Rejea: Uchaguzi wa Urais 1995, mgawanyo wa kura za Augustine Lyatonga Mrema)

Mizunguko ya kampeni huzaa kura za ziada mbali na zile za wanachama. Tayari inaonyesha kwamba Magufuli anapita karibu kila kata ya Tanzania akitumia barabara huku upande wa Lowassa na shirikisho la Ukawa hali ikiwa tofauti, ambako amekuwa akifika sehemu chache akitumia usafiri wa ndege na helkopta na ni wazi hana stamina ya kuzunguka kwa gari nchi nzima kutokana na tatizo la kiafya.

CCM ina mizizi kwenye mashina kuanzia ngazi ya nyumba kumi. Mtandao huu wa Chama pamoja na safari za mgombea wao kila kata ni kiashiria kwamba atafikia wapiga kura wengi zaidi hasa sehemu za vijijini na ambazo si rahisi kufikika. Tafiti zinaonyesha huko ndiko kwenye wapiga kura wengi na kuwafikia ni hatua moja kuelekea kuzipata kura zao na kushinda.

Chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2014 zinaonyesha kwamba CCM ilishinda kwa zaidi ya asilimia 80 kwenye nafasi za uongozi za serikali za vijiji na mitaa. Ikumbukwe kwamba CCM ilipata ushindi huu licha ya ushindani mkubwa uliokolezwa na sakata la Escrow wakati huo. Hii inaonyesha kwamba CCM iliweza kushinda hata wakati huo wa changamoto.

Ni mwaka mmoja tu umepita tangu chaguzi hizo zifanyike. Kitafiti, hiki ni kiashiria kikubwa kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CCM kama chama kinaenda kwenye sanduku la wapiga kura kikiwa na rekodi nzuri kuweza kushinda.

Babu wa Loliondo kaongea… tarajia hili kutoka kwake time hii!

Babu wa Loliondo 
Ambilikile Mwasapila maarufu kama Babu wa Loliondo ndio mmiliki wa hii post kwa leo, babu aliyejipatia umaarufu kwa kutoa dawa kwenye kikombe ambayo wengine walidai kupona magonjwa mbalimbali na wengine hawakupona baada ya kunywa kwenye miaka ya 2011 na 2012.
Kuanzia 2012 umaarufu wa Babu huyu aliefanya foleni ya watu kwenda kumuona kuchukua mpaka wiki tatu kutokana na wingi wa watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya na Zambia, ulianza kupotea na alipohojiwa na millardayo.com February 2013 alisema kuna muujiza mwingine unakuja watu wasubirie.
Kwenye Interview nyingine ya August 2015, Babu wa Loliondo ameibuka na kusema bado unakuja muujiza mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo na huu ndio utaleta watu wengi kutoka mataifa mbalimbali lakini hawezi kusema ni kitu gani sababu hajaruhusiwa na Mungu kusema.
Anasema ‘wengine watakuja kwa kunywa dawa, wengine watakuja kwa mambo mengine tu ikiwemo kuona maajabu, mwanzoni niliwaambia watu kwamba tutapata foleni kubwa sana hapa na hawakunielewi ila sasa wananielewa nikisema, hayo maajabu mapya yatakua kwa mfumo wa dawa na miujiza mingine ambayo Mungu hajaniruhusu kuitaja
Ambilikile Mwasapila ‘Babu wa Loliondo’ anasema ukimya wake umetokana na muongozo wa Mungu, ataendelea kuwa kimya mpaka Mungu atakapoufungua muujiza mwingine wa pili aliomuonyesha kwenye maono miaka kadhaa iliyopita, anajua kuna kitu kikubwa kinakuja ila sio muda wake kukisema sasa hivi.
Ameandaa heka 16 kwa ajili ya miujiza hii mikubwa ambapo hata 2013 aliionyesha millardayo.com shamba hilo kubwa aliloliandaa ikiwemo kujenga nyumba za kupokelea watu ambapo kwenye huu muujiza mpya anasema lengo lake sio hela sana kwani hata ile 500 aliyokua akiitoza kwenye muujiza wa kwanza ilikua ni agizo la Mungu na sio yeye, kama safari hii Mungu atasema iongezeke atafanya hivyo, akisema iwe bura ni sawa vilevile’
Babu wa Loliondo ambaye ana umri wa miaka 81 sasa hivi, ni baba wa watoto wanne ambapo wa kike ni mmoja na wakiume watatu, mke wake alifariki mwaka 2009.

Diamond Platnumz ametaja tarehe atakayoonekana sura mtoto wake (Tiffah)


Kama umekua ukifuatilia akaunti za Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari tangu mtoto wao Tiffah azaliwe utakua umekutana na picha nusu ambayo anaonekana mtoto wao huyo na sehemu kubwa hua ni kuanzia kwenye kidevu kushuka chini.
tifHii imekua ni style nyingine ya mastaa wetu kadhaa kuchukua mfumo huu wa kutowapost au kuwaonyesha watoto wao hadi umri fulani ufike,Diamond Platnumz leo ametaja siku ambayo mtoto wao huyo ataonekana sura kwa wale ambao bado hawajapata nafasi ya kumuon
Diamond kasema ayo katika ukurasa wake wa istagram.................................................
 On the 20th of September 2015 my Daughter's face @princess_tiffah will be Exclusively shown for the first time to the public... would you like to know which companies have sponsored her first video and photo??? Apart from being @MsasanicityMall and @PuguMall #BABYSHOP brand Ambassador would you like to know which companies have endorsed her??? Stay with me!!! #TIffahsDay Coming Soon..% (Tareh 20|09|2015 kwa mara ya kwanza sura ya Binti yangu @princess_tiffah tutaiweka hadharani...je ungependa kujua ni Kampuni gani imedhamini Video na Picha yake ya kwanza????.. Mbali na kuwa balozi wa #BABYSHOP ya @Msasanicitymall & @Pugumall ungependa kujua amekuwa Balozi wa nini tena???.. uskae mbali na mimi... #TiffahsDay inakaribia..%) #ProudDad

LOWASA AVUNJA REKODI SUMBAWANGA MJINI

Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukitoka Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga na kuelekea kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, Sepremba 2, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Ikuo Malila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini,  Sepremba 2, 2015.

Dj Gaby on the mix