Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Monday, 7 September 2015

SABABU 10 KWANINI JOHN MAGUFULI ATASHINDA UCHAGUZI MKUU WA URAISI 2015




Tanzania bara na visiwani yako majimbo ya uchaguzi 266, CCM imesimamisha wagombea Ubunge katika majimbo yote 266 huku Chadema na washirika wake wa Ukawa wakiwa wamesimamisha wagombea katika majimbo 211 (138 toka Chadema). Kati ya majimbo hayo 266, CCM tayari imepita bila kupingwa majimbo 7.

Ukichukua majimbo 259 yaliyobaki na kutoa 211 ambayo Chadema na washirika wake wamesimamisha wagombea unabaki na majimbo 48 ambayo CCM haina upinzani wa Chadema wala washirika wake wa Ukawa. Majimbo haya 48 CCM ina uhakika wa kushinda walau kwa asilimia 90, ushindi huu si kwa Wabunge tu bali pia kwa mgombea Urais wa CCM.

Watanzania waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2015 ni milioni 24.2. Takwimu zinaonyesha CCM ina wanachama hai wapatao milioni 8 wenye kadi na wanaolipia ada zao za uanachama kila mwaka. Kuondoka kwa Edward Lowassa katika Chama Cha Mapinduzi kunamaanisha Magufuli hatapata kura zote milioni 8 za wana CCM na pia kihesabu si rahisi wana CCM wote milioni 8 kujitokeza siku ya kupiga kura.

Utafiti unaonyesha kwamba wana CCM watakaopiga kura hawatazidi asilimia 90 ya wanachama wake (milioni 7.2) huku milioni 7 kati yao wakimpigia kura John Magufuli. Historia ya CCM inaonyesha ni wanachama wachache sana humpigia kura kada mwenzao anapohama kugombea nafasi kwa chama kingine, hasa nafasi ya Urais (Rejea: Uchaguzi wa Urais 1995, mgawanyo wa kura za Augustine Lyatonga Mrema)

Mizunguko ya kampeni huzaa kura za ziada mbali na zile za wanachama. Tayari inaonyesha kwamba Magufuli anapita karibu kila kata ya Tanzania akitumia barabara huku upande wa Lowassa na shirikisho la Ukawa hali ikiwa tofauti, ambako amekuwa akifika sehemu chache akitumia usafiri wa ndege na helkopta na ni wazi hana stamina ya kuzunguka kwa gari nchi nzima kutokana na tatizo la kiafya.

CCM ina mizizi kwenye mashina kuanzia ngazi ya nyumba kumi. Mtandao huu wa Chama pamoja na safari za mgombea wao kila kata ni kiashiria kwamba atafikia wapiga kura wengi zaidi hasa sehemu za vijijini na ambazo si rahisi kufikika. Tafiti zinaonyesha huko ndiko kwenye wapiga kura wengi na kuwafikia ni hatua moja kuelekea kuzipata kura zao na kushinda.

Chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2014 zinaonyesha kwamba CCM ilishinda kwa zaidi ya asilimia 80 kwenye nafasi za uongozi za serikali za vijiji na mitaa. Ikumbukwe kwamba CCM ilipata ushindi huu licha ya ushindani mkubwa uliokolezwa na sakata la Escrow wakati huo. Hii inaonyesha kwamba CCM iliweza kushinda hata wakati huo wa changamoto.

Ni mwaka mmoja tu umepita tangu chaguzi hizo zifanyike. Kitafiti, hiki ni kiashiria kikubwa kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CCM kama chama kinaenda kwenye sanduku la wapiga kura kikiwa na rekodi nzuri kuweza kushinda.

No comments:

Post a Comment