Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Tangaza nasi DvJGaby.Blogspot,com

Friday, 30 October 2015

SUPER STAR DIAMOND PLATNUMZ KUWEKA HISTORIA ULAYA

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Andrew Carlos na Musa Mateja
OKTOBA 25, mwaka huu ilikuwa ni moja kati ya siku za kihistoria nchini kwa Watanzania wote kujumuika na kupiga kura za kuwachagua wabunge, madiwani na rais.
Siku hiyohiyo pia katika Jiji la Milan, Italia kulikuwa na tukio la kihistoria kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla katika Tuzo za MTV Europe Music (EMA) na kufanikiwa kuibuka na ushindi kupitia kipengele cha Best Worldwide Act: Africa/India ambacho alikuwa akichuana na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia Miss World mwaka 2000.
Uso kwa uso na mastaa ulaya 


Kati ya matukio ambayo Diamond anasema hawezi kuyasahau ni pamoja na kupata shavu la kukutana na mastaa kibao wa ulaya ambao walipafomu na wengine kuchukuwa tuzo. 

“Nimekutana na mastaa wengi ambao sikuwahi kukutana nao kabisa zaidi ya kuwaona tu kwenye mitandao na TV. Mastaa hao ni pamoja na Jason Deluro ambaye pia alipafomu Wimbo wa Want to Want, Pharrel Williams naye alipafomu Wimbo wa Freedom.“Nilipata bahati pia ya kuwashuhudia mastaa wengine kama vile Justin Bieber, Ed Sheeran na wengine kibao,” alisema Diamond. 

Bieber anyakua 5 kwa mpigo 
Staa wa Pop, Justin Bieber aliweka historia kwake katika tuzo hizo baada ya kuibuka na tuzo tano kwa mpigo.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao. 

Wazungu wapagawa na Diamond 
Katika hali ya kushangaza mapema kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za utoaji tuzo, Diamond aliyekuwa amevalia suti nyeupe alitinga ‘red carpet’ na kushangaa kuvamiwa na wazungu waliookuwa wamepanga foleni kuwasubiri mastaa huku kila mmoja akiwa na simu yake mkononi akitaka kupiga picha naye (selfie). 

Washindi waliopita 
Katika kipengele alichoshinda Diamond, alitanguliwa na Abdelfattah Grini (Morocco) aliyechukuwa mwaka 2011, Ahmed Soultan (Morocco) mwaka 2012 na 2013 na wa mwisho alikuwa Mohamed Assaf (Palestina). 

Diamond anasemaje? 
Kutokana na ushindi huo uliokuja Tanzania na Afrika kwa ujumla, Diamond alifunguka mengi ya kushukuru kwa wale wote waliompigia kura na kuahidi kufanya makubwa zaidi ya hayo katika kazi zake za muziki. 

“Nimeshangazwa sana kwa namna ambayo nimepokelewa kwa kishindo nchini Italia. Wazungu wamenionesha thamani ya juu kwa mapokezi makubwa na kunishangilia na kunipongeza kwa tuzo niliyoipata. Nasema asanteni sana Watanzania wenzangu kwa sapoti mlionionesha mwanzo mwisho hadi kwa kunipigia kura na kufanikiwa kuibuka mshindi kutoka Afrika,” alisema Diamond. 

Diamond alifanikiwa kupita tano bora Afrika katika Tuzo za Ema baada ya kupigiwa kura za kutosha na mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter. Wasanii wa Afrika aliokuwa akichuana nao kabla ya kutua Italia ni Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na Wizkid (Nigeria).

ZARI THE BOSS LADY AFANYA UAMUZI MGUMU KWA MWANAE TIFFAH


NA HAMIDA HASSAN
DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi wabaki na vingi viulizo.
Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo.

Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’ hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.

Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.

Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’ hiyo na nyingine hana.
Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa.

“Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake, alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo hayo hayapo. Kitendo cha yeye kwenda Sauzi na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau, amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo sawa,” alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.
Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo

Magazeti leo october 30 ijumaa







.................DSC01871...

Dr. Magufuli Akabidhiwa Rasmi CHETI Cha Ushindi wa Kiti cha Urais


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha urais, Dk John Pombe Magufuli  na  mgombea  mwenza  wake  Samia  Suluhu  katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee  asubuhi  hii.
Katika  tukio  hilo, Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wamesusia sherehe hizi  za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM. 

DvJ Gaby Blog

Baada ya Dk. Magufuli kutangazwa mshindi, yajue haya ya Lowassa.

low

Thursday, 29 October 2015

Rais Kikwete Alivyomkaribisha Kumpongeza Dk. Magufuli Baada ya Matokeo ya Urais Kutangazwa

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni  jana  jioni Oktoba 29, 2015
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jana jioni Oktoba 29, 2015



Mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea salamu za pongezi kutoka kwa mgombea Urais Mwanamke Pekee kwa tiketi ya ACT Wazlendo Mama Anna Mghira mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jana jioni Oktoba 29, 2015

Breaking News: Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania kwa Asilimia 58.46


Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva   imemtangaza  Rasmi  mgombea  Urais  wa  CCM, Dr John Pombe  Magufuli  kuwa  mshindi  halali  wa  kiti  cha  Urais  katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.  

Kwa  Mujibu  wa  jaji  Lubuva, Dr  magufuli  amepata  ushindi  wa  kura Milioni 8 ( 8,882,935  ) sawa  na  asilimia  58.46%  huku  akimwacha  kwa  mbali  mpinzani  wake  wa  karibu , Edward  Lowassa (Chadema )  ambaye  amepata  jumla  ya  kura  Milioni 6 (  6,077,848  )  sawa  na  asilimia  39.97%
Dr  Magufuli  na  mgombea  mwenza, Samia Suluhu  watakabidhiwa  rasmi  vyetu  vya  ushindi  kesho  saa  nne  asubuhi  katika  ukumbi  wa  hoteli  ya  Diamond  Jubilee  

Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais


Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.

• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.

Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani

Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
 
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.

Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.

Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015
DJ GABY BLOG

Maneno ya kwanza ya Profesa Jay baada ya kushinda kiti cha Ubunge.

Bado tupo kwenye headlines za uchaguzi 2015 ambapo msanii mkongwe wa HipHop Tanzania Joseph Haule (Profesa Jay) ni mmoja wa wawashindi wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi huu akiwa amechukua jimbo la Mikumi Morogoro na anachosubiri kwa sasa ni kuingia bungeni.
Prof. ameongea na millardayo.com >>>‘Nawashukuru sana wananchi wa Mikumi kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa, watanzania wameniamini kwa sababu ya upeo mkubwa ambao Mungu amenipa, naamini sana katika umoja na mshikamano….! na ndiomaana nimekuwa nasisitiza hata katika kampeni zangu, lazima tushikamane watu wote wa vyama vyote na hata wasio na vyama ili kuikomboa Mikumi yetu ‘ –
.
.
Changamoto kubwa ni maji, elimu, miundo mbinu pamoja na ajira, nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu kwasababu wao ndio wamenituma Dodoma, mimi kuwa mwanamuziki halitonizuia kuwawakilisha wananchi…. nitaendelea kuwa mwanamuziki na huwenda nikafanya muziki ule wa juu zaidi kwasababu nategemea kukutana na watu wa juu zaidi’

Mgombea mwenza wa CHADEMA Juma Duni Haji Akatazwa Kuingia katika Chumba cha Kutangazia Matokeo ya Urais


Mgombea mwenza wa CHADEMA Juma Duni Haji amezuiwa kuingia katika chumba cha kutangazia matokeo ya urais katika ukumbi wa Julius Nyerere wakati zoezi hilo likiendelea baada ya kueleza kuwa ameleta hati ya pingamizi ya matokeo.

Hata hivyo walinzi wa eneo la kutangazia matokeo walimkatalia kuingia katika chumba hicho na kumtaka aende Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchguzi (NEC) kuwasilisha hati yake hiyo na kisha kusindikizwa kwenye gari alilokuja nalo lenye namba T754 DDY aina ya Toyota.
DvJGABY.BLOG

Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini Wapinga Uchaguzi Mkuu Kufutwa Zanzibar


Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini umetoa taarifa ukipinga kufutiliwa mbali kwa matokeo ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar.
 
Ubalozi huo umesema kuwa hauoni sababu za kufutiliwa mbali kwa matokeo hayo ilhali waangalizi walifurahishwa na vile uchaguzi huo ulivyofanyika kwa amani.
 
Wameitaka tume ya uchaguzi Kiswani Zanzibar kuorodhesha matokeo hayo bila kuchelewa.
----------------------------
PRESS STATEMENT
Thursday 29 October, 2015

United Kingdom statement on Zanzibar elections

The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland is deeply concerned by the announcement of the Chairman of the Zanzibar Electoral Commission to nullify the elections. We note that all the international observers were impressed by the quality of the electoral process they witnessed. We call on ZEC to resume the results tabulation process without delay.

We congratulate the people of United Republic of Tanzania on the peaceful and enthusiastic way in which they participated in their elections.We call on all political actors to seek a solution which respects the will of the Zanzibari people as expressed in the polls on 25 October.

The United Republic of Tanzania has a well deserved reputation for peace and stability and respecting democratic principles. We urge all Zanzibaris to maintain peace and we commend the restraint they have shown so far.
Dj Gaby Blog.

Breaking News: Tume ya Uchaguzi Zanzibar imefuta Matokeo yote ya Uchaguzi mkuu Zanzibar.


Tume  ya  Uchaguzi  Zanzibar  imeufuta uchaguzi  mkuu wa  Zanzibar  kutokana  na  kuwa  na  dosari  nyingi  ikiwemo uchaguzi  kutokuwa  huru  na  wahaki 

Mwenyekiti  wa  ZEC  amewaambia  waandishi  wa  habari   mchana  huu  kuwa  amechukua  maamuzi  hayo  baada  ya  kujiridhisha  kuwa  uchaguzi  uligubikwa  na  dosari  nyingi.

"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa....
 
"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"! - Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Marekani Yalaani Kufutwa kwa Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar


Marekani imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani humo.

Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa ubalozi huo nchini Tanzania, Marekani ilisema imeshtushwa na hatua hiyo na kutoa wito tume hiyo iondoe tamko hilo.

Zec imeahidi kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.

Katika kufutilia mbali matokeo ya urais wa Zanzibar, tume ya uchaguzi ya Zanzibar-ZEC ilisema shughuli nzima ya upigaji kura visiwani iligubikwa na kasoro nyingi.


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha alisema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".

"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."


Alisema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura".


Kadhalika, alisema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako alisema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.

Hata hivyo, taarifa ya ubalozi wa Marekani inasema kufutilia mbali matokeo hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.

Aidha Taarifa hiyo inasema kuwa hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi kutoka ubalozi wa Marekani, jumuiya ya ulaya, jumuiya ya madola na jumui ya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki.

Wednesday, 28 October 2015

LIVE: Matokeo Rasmi ya Urais kwa Mujibu wa NEC (Official Results) - Uchaguzi Mkuu 2015


Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Urais kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa.

Tembelea  ukurasa huu mara kwa mara  kwa updates zaidi
  ==================================
 October 28, 2015 - Saa 10 jioni
Lubuva: " Hadi sasa tumefikisha Majimbo 195, bado majimbo 69 na tutamaliza kesho, kisha mshindi atapewa cheti cha ushindi"
 
1. URAIS Jimbo TEMEKE
CCM: 106,612
CHADEMA: 124,274
 
2. URAIS Jimbo RUFIJI
CCM - 21,714
CHADEMA - 18,308
 
3. URAIS Jimbo KIBITI
CCM: 21,142
CHADEMA: 18,629
 
4. URAIS Jimbo MBARALI
CCM: 55,933
CHADEMA: 45,374
 
5. URAIS Jimbo BARIADI
CCM: 85,813
CHADEMA: 57,922
 
6. URAIS Jimbo GEITA MJINI
CCM - 43,576
CHADEMA - 25,030
 
7. URAIS Jimbo UBUNGO
CCM: 71,928
CHADEMA: 83,637
 
8. URAIS Jimbo BUSOKELO
CCM: 18,834
CHADEMA: 12,596
 
9. URAIS Jimbo KWELA
CCM: 49,196
CHADEMA: 32,980
 
10. URAIS Jimbo MOROGORO KUSINI
CCM: 35,505
CHADEMA: 13,586
 
11. URAIS Jimbo KARAGWE
CCM: 62,159
CHADEMA: 41,676
 
12. URAIS Jimbo MUHEZA
CCM: 53,237
CHADEMA: 22,635
 
13. URAIS Jimbo ILALA
CCM: 37,329
CHADEMA: 36,330
 
14. JimboBUBUBU
CCM: 10,026
CHADEMA: 7,332
 
15. RAIS Jimbo TABORA MJINI
CCM: 52,906
CHADEMA: 30,027
 
16. URAIS Jimbo ARUMERU MASHARIKI
CCM: 31,040
CHADEMA: 88,912
 
17. URAIS Jimbo NYAMAGANA
CCM: 99,890
CHADEMA: 78,329
 
18. URAIS Jimbo MTWARA MJINI
CCM: 25,828
CHADEMA: 30,195
 
19. URAIS Jimbo BUKOBA VIJIJINI
CCM: 64,839
CHADEMA: 32,346
 
20. URAIS Jimbo SONGWE
CCM: 30,778
CHADEMA: 14,738
 
21. URAIS Jimbo CHEMBA
CCM: 51,594
CHADEMA: 20,800
 
22. URAIS Jimbo BUCHOSA
CCM: 62,762
CHADEMA: 31,660
 
23. URAIS Jimbo KILWA KASKAZINI
CCM: 17,553
CHADEMA:14,722
 
24. URAIS Jimbo KIBAKWE
CCM: 36,830
CHADEMA: 8,018
 
25. URAIS Jimbo KILWA KUSINI
CCM: 18,767
CHADEMA: 22,377
 
26. URAIS Jimbo MOROGORO KUSINI MASHARIKI
CCM: 30,624
CHADEMA: 13,304
 
27. URAIS Jimbo HANANG
CCM: 63,205
CHADEMA: 32,367
 
28. URAIS Jimbo MOROGORO MJINI
CCM: 85,440
CHADEMA: 65,580
 
29. URAIS Jimbo KIGAMBONI
CCM: 35,735
CHADEMA: 39,754
 ====================================
October 28, 2015 - Saa 4 Asubuhi

 Jimbo  la  Lupa-Mbeya

Magufuli (CCM):37,684
Lowassa (CHADEMA): 20,175 

 Jimbo  la  Lushoto-Tanga

Magufuli (CCM):28,058
Lowassa (CHADEMA): 8,673

 Jimbo  la  Musoma Mjini-Mara

Magufuli (CCM):33,658
Lowassa (CHADEMA): 25,352

 Jimbo  la  Mvomero-Morogoro

Magufuli (CCM): 68,179
Lowassa (CHADEMA):33,468

 Jimbo  la  Hai-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 29,341
Lowassa (CHADEMA):49,125

 Jimbo  la  Bukombe-Geita

Magufuli (CCM):50,063
Lowassa (CHADEMA): 28106

 Jimbo  la Iringa Mjini

Magufuli (CCM):  36,584
Lowassa (CHADEMA):38,860

 Jimbo  la  Bagamoyo

Magufuli (CCM):29,969
Lowassa (CHADEMA):16,245

 Jimbo  la  Sumbawanga mjini-Rukwa

Magufuli (CCM):43,542
Lowassa (CHADEMA): 34,201


 Jimbo  la Same Mashariki-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 18,520
Lowassa (CHADEMA):17,874

Jimbo la Mlalo
Magufuli (CCM): 33,996
 
Lowassa  (Chadema): 8,938
 
Jimbo la Kishapu
Kura:86,125

Magufuli (CCM):65,173
Lowassa  (Chadema):17,177
 

  Jimbo la Msalala
Kura:64,111

 Magufuli(CCM):44,213
 Lowassa  (Chadema):16,942
 

 Jimbo la Ludewa
Kura: 48,499
 
Magufuli (CCM):35,365 
Lowassa (Chadema):11,715

Jimbo la Tarime Mjini
Kura: 35,060
 
Magufuli(CCM): 18,009
Lowassa   (Chadema): 15,992

Jimbo la Mtwara Vijijini
Kura: 51,233

 Magufuli (CCM):25,938
 Lowassa   (Chadema):24,518
 

 Jimbo la Busanda
Kura:114,955
 
Magufuli(CCM):73,834 
Lowassa   (Chadema):35,373
 

  Jimbo la Ushetu
Kura: 76,757
 
Magufuli (CCM):51,034 
Lowassa   (Chadema):21,585

Jimbo la Shinyanga Mjini
Kura:68,745
 
Magufuli (CCM): 41,692
 Lowassa   (Chadema):25,465

Jimbo la Mbogwe
Kura: 58,837
 
Magufuli (CCM):44,558
 Lowassa   (Chadema):12,040

Jimbo la Kasulu Mjini
Kura: 52,670
 
Magufuli (CCM): 32,297 
Lowassa   (Chadema): 15,762
 

 Jimbo la Mlimba
Kura:76,182
 
Magufuli (CCM): 39,555 
Lowassa   (Chadema):35,994

 Jimbo la Mikumi
Kura: 65,241

Magufuli(CCM):35,192 
Lowassa   (Chadema):26,841

 Jimbo la Kilosa
Kura: 83,679

Magufuli (CCM):55,839
Lowassa   (Chadema):24,276

Jimbo la Bukoba Mjini
Kura: 53,710

Magufuli (CCM): 27,620
 Lowassa   (Chadema): 25,898

Jimbo la Moshi Vijijini
Kura: 82,782

Magufuli (CCM): 25,017 
Lowassa  (Chadema): 54,823

Jimbo la Sengerema
Kura:104108

Magufuli (CCM):69392
 Lowassa  (Chadema):28335

Matokeo ya Urais, Jimbo la Tunduma
Kura:52,797

 Magufuli (CCM):19,446 
Lowassa  (Chadema):32,219

Matokeo ya Urais, Mufindi Kaskazini
Kura:36,076
 
Magufuli(CCM):26,412 
Lowassa  (Chadema):8,085

Matokeo ya Urais, Jimbo la Nysa
Kura: 46,551
 
Magufuli(CCM):30,609 
Lowassa   (Chadema):14,062

Matokeo ya Urais, Jimbo la Isimani
Kura:42,933
 
Magufuli(CCM):26,766 
Lowassa  (Chadema):15,303

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kavuu
Kura: 30,813

 Magufuli (CCM): 21,483 
Lowassa   (Chadema): 8,083

Matokeo ya Urais, Mpanda Mjini
Kura: 50,623
 
Magufuli(CCM): 32,770 
Lowassa   (Chadema): 16,569

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kalenga
Kura:58,932
 
Magufuli (CCM):40,896 
Lowassa   (Chadema):16,890

Matokeo ya Urais, Jimbo la Rombo
Kura:82,862
 
Magufuli (CCM): 21,908
 Lowassa   (Chadema): 57,715

Matokeo ya Urais, Kahama Mjini
Kura: 89,961
 
Magufuli(CCM): 58,728
 Lowassa  (Chadema): 27,501

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kwimba
Kura: 53,760
 
Magufuli(CCM):40,544 
Lowassa  (Chadema):10,071

Matokeo ya Urais, Jimbo la Magu
Kura: 105,804
 
Magufuli(CCM):69,991
 Lowassa  (Chadema):30,070

Matokeo ya Urais, Jimbo la Geita
Kura: 69,778
 
Magufuli(CCM): 45,472 
Lowassa (Chadema):18,640

Matokeo ya Urais, Jimbo la Chato
Kura: 117,485
 
Magufuli(CCM):83,820 
Lowassa  (Chadema):27,936

Matokeo ya Urais, Jimbo la Bahi
Kura: 67,993

 Magufuli (CCM): 51,138 
Lowassa (Chadema): 11,340

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kilombero
Kura:99,255
 
Magufuli(CCM):49478
 Lowassa  (Chadema):49166

Matokeo ya Urais, Mbinga Vijijini
Kura: 72,545
 
Magufuli (CCM):55,895 
Lowassa  (Chadema):12,213

Matokeo ya Urais, Jimbo la Sumve
Kura: 46,293
 
Magufuli (CCM): 32,079 
Lowassa (Chadema):11,203

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kalambo
Kura:70,575
 
Magufuli(CCM):38,165 
Lowassa  (Chadema):29,507

Matokeo ya Urais, Jimbo la Busega
Kura:70,664

 Magufuli (CCM):47,049
 Lowassa (Chadema):19,765

Matokeo ya Urais, Jimbo la Kilolo
Kura: 82,079
 
Magufuli (CCM):52,517 
Lowassa  (Chadema):25,424

Matokeo ya Urais, Jimbo la Gairo
Kura: 54,157
 
Magufuli (CCM): 44,659
 Lowassa  (Chadema):6,925

Matokeo ya Urais, Jimbo la Liwale
Kura: 44360

 Magufuli(CCM):19,967
 Lowassa  (Chadema): 23,176

===========================================
 October 27, 2015 - Saa 2 Usiku
 
 Jimbo  la  Mfenesini-Mjini Magharinibi

Magufuli (CCM): 4496
Lowassa (CHADEMA): 3047

Jimbo  la  Mahonda

Magufuli (CCM): 4760
Lowassa (CHADEMA): 1449

Jimbo  la  Rungwe-Mbeya

Magufuli (CCM): 47,862
Lowassa (CHADEMA):41,534

Jimbo  la  Arumeru  Magharibi-Arusha

Magufuli (CCM): 27,658
Lowassa (CHADEMA): 105,720

Jimbo  la  Pangani-Tanga

Magufuli (CCM):14,041
Lowassa (CHADEMA): 10,151

Jimbo  la  Korogwe Vijijini-Tanga

Magufuli (CCM):  51,984
Lowassa (CHADEMA):19,050

Jimbo  la  Kijito Upele-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):  8,075
Lowassa (CHADEMA):5,639

Jimbo  la  Chahali-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 4689
Lowassa (CHADEMA):2585
  
Jimbo  la  Kiembe Samaki

Magufuli (CCM): 6618
Lowassa (CHADEMA): 5610

Jimbo  la  Chahali-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 4689
Lowassa (CHADEMA):2585

Jimbo  la  Manyoni Magharibi-Singida

Magufuli (CCM): 24,675
Lowassa (CHADEMA): 9901
 
Jimbo  la  Iramba Magharibi-Singida

Magufuli (CCM): 50,322
Lowassa (CHADEMA):11,714
 
Jimbo  la  Dimani-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM): 5,292
Lowassa (CHADEMA): 1,861

Jimbo  la  Nzega-Tabora

Magufuli (CCM): 18,843
Lowassa (CHADEMA):10,195

Jimbo  la  Igunga-Tabora

Magufuli (CCM): 36,796
Lowassa (CHADEMA):18,600
 
Jimbo  la  Urambo  Mashariki-Tabora

Magufuli (CCM): 36,458
Lowassa (CHADEMA): 22,385

Jimbo  la Babati Vijijini-Manyara

Magufuli (CCM): 67,183
Lowassa (CHADEMA): 42,334

Jimbo  la  Kiteto-Manyara

Magufuli (CCM): 41,862
Lowassa (CHADEMA): 31,268

Jimbo  la  Bukene-Tabora

Magufuli (CCM):36,229
Lowassa (CHADEMA): 11,380

Jimbo  la  Sikonge-Tabora

Magufuli (CCM): 36,729
Lowassa (CHADEMA):16,164
 
Jimbo  la  Kaliua-Tabora

Magufuli (CCM): 28,599
Lowassa (CHADEMA): 19,724

Jimbo  la  Ulyankulu-Tabora

Magufuli (CCM): 35,329
Lowassa (CHADEMA):7,568

Jimbo  la  Kyela-Mbeya

Magufuli (CCM): 44,451
Lowassa (CHADEMA):37,563

Jimbo  la  Manonga-Tabora

Magufuli (CCM):32,013
Lowassa (CHADEMA): 14,343

Jimbo  la  Ukerewe-Mwanza

Magufuli (CCM): 55,091
Lowassa (CHADEMA):47,667

Jimbo  la  Dodoma-Mpwapwa

Magufuli (CCM):37,480
Lowassa (CHADEMA):8,230

Jimbo  la  Longido-Arusha

Magufuli (CCM):14,621
Lowassa (CHADEMA): 25,361

Jimbo  la  Kondoa Mijini-Dodoma

Magufuli (CCM):15,113
Lowassa (CHADEMA): 7,102

 ===================================
 October 27, 2015 - Saa 8.40 Mchana

Jimbo  la  Fuoni-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM): 956
Lowassa (CHADEMA):420

Jimbo  la  Kikwajuni-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6,317
Lowassa (CHADEMA): 3669

 Jimbo  la  Mpanda Vijijini-Katavi

Magufuli (CCM):37,321
Lowassa (CHADEMA): 12,791

Jimbo  la  Mchinga-Lindi

Magufuli (CCM):13,948
Lowassa (CHADEMA):12,936

Jimbo  la  Mwela-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6430
Lowassa (CHADEMA):5865

Jimbo  la Nkasi  Kaskazini-Rukwa

Magufuli (CCM):25,837
Lowassa (CHADEMA):19,891

Jimbo  la  Nkasi Kusini-Rukwa

Magufuli (CCM): 21,572
Lowassa (CHADEMA): 13,550


Jimbo  la  Nkenge-Kagera

Magufuli (CCM): 42,568
Lowassa (CHADEMA): 25,840

Jimbo  la  Amani-Kusini Magharibi

Magufuli (CCM):4,322
Lowassa (CHADEMA):3,157

Jimbo  la  Bumbwini

Magufuli (CCM):2503
Lowassa (CHADEMA): 2822

Jimbo  la  Nungwi- Mkoa wa Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM):4135
Lowassa (CHADEMA): 4853

Jimbo  la Uzini

Magufuli (CCM):6537
Lowassa (CHADEMA):1864

Jimbo  la  Chwaka

Magufuli (CCM):6537
Lowassa (CHADEMA): 1864

Jimbo  la Mtama-Lindi

Magufuli (CCM):29,625
Lowassa (CHADEMA):20,841

Jimbo  la Tunguu-Kusini Unguja

Magufuli (CCM): 8,519
Lowassa (CHADEMA): 2,923

Jimbo  la Biharamuro-Kagera

Magufuli (CCM):44,943
Lowassa (CHADEMA):28,576

Jimbo  la Arusha Mjini-Arusha

Magufuli (CCM): 65,107
Lowassa (CHADEMA): 150,786

Jimbo  la Chake Chake

Magufuli (CCM):1253
Lowassa (CHADEMA):5209

Jimbo  la Kibaha Vijijini-Pwani

Magufuli (CCM):20,805
Lowassa (CHADEMA):11,344

Jimbo  la Mwanakwereke

Magufuli (CCM): 4206
Lowassa (CHADEMA):4606

Jimbo  la Nachingwea-Lindi

Magufuli (CCM):46,485
Lowassa (CHADEMA):30,252

Jimbo  la Mafya- Pwani

Magufuli (CCM): 11,153
Lowassa (CHADEMA):9,363

Jimbo  la Mkuranga- Pwani

Magufuli (CCM):45,710
Lowassa (CHADEMA): 36,478

Jimbo  la Welezo

Magufuli (CCM):2615
Lowassa (CHADEMA):2582

Jimbo  la Magomeni-Kusini Magharibi

Magufuli (CCM): 5716
Lowassa (CHADEMA):3711
  == ===================================
October 27, 2015 - Saa 3 Asubuhi  
 
Jimbo  la  Chalinze

Magufuli (CCM):52,212
Lowassa (CHADEMA):21380

Jimbo  la  Chonga

Magufuli (CCM):1740
Lowassa (CHADEMA):3800
 
Jimbo  la  Chumbuni

Magufuli (CCM): 5096
Lowassa (CHADEMA): 4450

Jimbo  la Ileje

Magufuli (CCM):26,368
Lowassa (CHADEMA): 15,651

Jimbo  la Kijini

Magufuli (CCM): 2703
Lowassa (CHADEMA): 3351

Jimbo  la Kilindi-Tanga

Magufuli (CCM): 33,942
Lowassa (CHADEMA):12,123
 
Jimbo  la Korogwe Mjini-Tanga

Magufuli (CCM): 17,168
Lowassa (CHADEMA): 9034

Jimbo  la Kohani-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6,245
Lowassa (CHADEMA): 2689


Jimbo  la Lupembe-Njombe

Magufuli (CCM): 23,061
Lowassa (CHADEMA): 7,466

Jimbo  la Madaba-Ruvuma

Magufuli (CCM): 13,949
Lowassa (CHADEMA):4,735

Jimbo  la Masasi Mjini-Mtwara

Magufuli (CCM): 24,637
Lowassa (CHADEMA):16,778

Jimbo  la Mbeya Vijijini-Mbeya

Magufuli (CCM):62,662
Lowassa (CHADEMA):47,038

Jimbo  la Mkwajuni-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 4,686
Lowassa (CHADEMA): 3,314

Jimbo  la Momba- Mbeya

Magufuli (CCM): 28,978
Lowassa (CHADEMA):24,418

Jimbo  la Monduli-Arusha

Magufuli (CCM):11,355
Lowassa (CHADEMA): 49,675

Jimbo  la Mpendae- Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):4,192
Lowassa (CHADEMA): 4,048

Jimbo  la Mwanga-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 25,738
Lowassa (CHADEMA):15,148

Jimbo  la Namtumbo-Ruvuma

Magufuli (CCM):44,061
Lowassa (CHADEMA): 23,039

Jimbo  la Newala Mjini-Mtwara

Magufuli (CCM): 21,269
Lowassa (CHADEMA):16,980

Jimbo  la Newala Vijijini-Mtwara

Magufuli (CCM): 29,799
Lowassa (CHADEMA): 13,958

Jimbo  la Siha-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 18,252
Lowassa (CHADEMA):22,572

Jimbo  la Solwa-Shinyanga

Magufuli (CCM): 66,096
Lowassa (CHADEMA): 23,510

Jimbo  la Tandahimba

Magufuli (CCM): 49,098
Lowassa (CHADEMA):46,288
  
Jimbo  la Tumbatu-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 5,720
Lowassa (CHADEMA):  3,967

Jimbo  la Igalula-Tabora

Magufuli (CCM): 28,747
Lowassa (CHADEMA): 8,393

Jimbo  la Ulanga-Morogoro

Magufuli (CCM):32,297
Lowassa (CHADEMA):20,489

Jimbo  la Wawi-Kusini Pemba

Magufuli (CCM): 1,748
Lowassa (CHADEMA): 5,216

Jimbo  la Ziwani-Kusini Pemba

Magufuli (CCM): 592
Lowassa (CHADEMA):6,067

Jimbo  la Ole-Kusini Pemba

Magufuli (CCM):681
Lowassa (CHADEMA):5,251
  
Jimbo  la .....-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 5,592
Lowassa (CHADEMA): 1,019

Jimbo  la Tabora Kaskazini-Tabora

Magufuli (CCM): 38,050
Lowassa (CHADEMA): 12,410

Jimbo  la Ruangwa

Magufuli (CCM): 34,516
Lowassa (CHADEMA): 26,827

Jimbo  la Malindi-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM): 2,581
Lowassa (CHADEMA): 5,662

Jimbo  la Jang'ombe-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM): 6,567
Lowassa (CHADEMA):2,839

Jimbo  la Mhambwe-Kigoma

Magufuli (CCM): 37,746
Lowassa (CHADEMA): 22,804

===============================
Oktoba 26, 2015 - Saa 4 asubuhi:

Jimbo la Makunduchi:

Magufuli (CCM): 8,406
Lowassa (CHADEMA): 1,769

Jimbo la Paje:

Magufuli (CCM): 6,035
Lowassa (CHADEMA): 1,899

Jimbo la Lulindi:

Magufuli (CCM): 31,603
Lowassa (CHADEMA): 11,543

October 26, 2015 - Saa 11 Jioni
Jimbo la Mkoani:

Magufuli (CCM): 3341
Lowassa (CHADEMA): 7368

Jimbo la Ndanda:

Magufuli (CCM): 33699
Lowassa (CHADEMA): 19017

Jimbo la Kiwengwa:

Magufuli (CCM): 3317
Lowassa (CHADEMA): 1104

Jimbo la Nsimbo:

Magufuli (CCM): 31413
Lowassa (CHADEMA): 6042

Jimbo la Mtambile:

Magufuli (CCM): 902
Lowassa (CHADEMA): 5875

Jimbo la Donge:

Magufuli (CCM): 5592
Lowassa (CHADEMA): 1019

Jimbo la Kiwani:

Magufuli (CCM): 1661
Lowassa (CHADEMA): 4229

Jimbo la Chambani:

Magufuli (CCM): 818
Lowassa (CHADEMA): 5319

Jimbo la Kibaha Mjini:

Magufuli (CCM): 34604
Lowassa (CHADEMA): 25448

Jimbo la Bumbuli:
Magufuli (CCM): 35310
Lowassa (CHADEMA): 7928

October 26, 2015 - Saa 2 Usiku
Jimbo la Gando:

Magufuli (CCM): 881
Lowassa (CHADEMA): 5903

Jimbo la Kisarawe:

Magufuli (CCM): 24086
Lowassa (CHADEMA): 13093

Jimbo la Kojani:

Magufuli (CCM): 1561
Lowassa (CHADEMA): 9982

Jimbo la Mbinga Mjini:

Magufuli (CCM): 29295
Lowassa (CHADEMA): 11695

Jimbo la Mgogoni:

Magufuli (CCM): 710
Lowassa (CHADEMA): 6506

Jimbo la Mkinga:

Magufuli (CCM): 23798
Lowassa (CHADEMA): 15142

Jimbo la Moshi Mjini:

Magufuli (CCM): 28909
Lowassa (CHADEMA): 49379

Jimbo la Mtambwe:

Magufuli (CCM): 428
Lowassa (CHADEMA): 6937

Jimbo la Nanyamba:

Magufuli (CCM): 24904
Lowassa (CHADEMA): 16992

Jimbo la Peramiho:

Magufuli (CCM): 32505
Lowassa (CHADEMA): 11291

Jimbo la Wete:
Magufuli (CCM): 958
Lowassa (CHADEMA): 5119
Jimbo la Singida Mjini

Kura: 56,558 

Magufuli (CCM): 36,035 

Edward Lowassa (Chadema): 19,007

Jimbo la Lindi Mjini 
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607
 
Jimbo la Njombe Mjini 
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368

=====================