
Zimepita siku chache tu toka Justin Bieber atangaze kuanza kwa tour yake ‘Purpose world tour ‘ mwanzoni wa mwaka 2016, tour itakayompeleka nchi 56 kwa ajili ya kuitangaza Album yake mpya, PURPOSE.
Licha ya ticket za tour hiyo kuuzwa bei ya juu, mitandao mingi Marekani imekuwa ikiripoti kasi ya ticket hizo kununuliwa huku wengine wakisema mwaka 2015 umeishia kuwa mwaka poa sana kwa Justin Bieber… Lakini kingine kikubwa cha kujua kuhusu tour hii ni package special ya VIP Selfie itakayopatikana kwenye tour ya Justin itakayo anza mwezi March mwaka 2016!

Kwa mujibu wa Altitude Tickets, package ya ticket za ‘I’ll Show You VIP #Purpose Experience’ zitauzwa kwa USD $925 ambayo ni sawa na milion 1,850,000, na mtu atakapo nunua package hiyo itamaanisha kuwa ataweza tu kupiga picha moja ya pamoja (Group Selfie) na Justin Bieber na kushare na watu wako kwenye Instagram… cha kushangaza zaidi ni kwamba package hii ya ticket zimeshakwisha tayari, yani SOLD OUT!!
No comments:
Post a Comment