Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba amenusurika kifo ajalini.
Dk. Kijo-Bisimba alipata ajali mbaya ya gari katika daraja la Salender Dar es Salaam jana.
Katika ajali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba anadaiwa kuvunjika mguu mmoja baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kupinduka mara nne.
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi wakati akitoka kusali eneo la
Posta akitumia gari dogo ya Toyota Prado namba T 159 ATY.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa LHRC, Ezekiel Masanja alisema baada
ya kupata taarifa ya ajali hiyo alikwenda na kumchukua Dk.
Kijo-Bisimba.
Alisema alimpeleka katika Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Masanja alisema vipimo vya awali vilionyesha amevunjika mguu lakini
hadi jana jioni madaktari walikuwa wakiendelea kumuangalia zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alikiri kutokea
tukio hilo akisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.
“Sina maelezo yanayojitokeza kuhusu ajali hii kwa sababu askari
wanaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo chake,”alisema Wambura.
Mashuhuda walisema gari la Dk. Kijo-Bisimba liligongwa ubavuni na
gari nyingine iliyokua inatoka la Sea View kwenda barabara ya Ali
Hassan Mwinyi.
Walisema gari hilo lilikua linaendeshwa na kijana ambaye hakufahamika
na baada ya kuligonga gari la Kijo-Bisimba lilizunguka mara nne na
kupinduka.
No comments:
Post a Comment