
Ni mwaka wa Watanzania kuzikusanya tuzo mbalimbali kwenye majukwa makubwa ya burudani Africa… Baada ya Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Ommy Dimpozkuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye tuzo za AFRIMMA 2015 zilizofanyika Dallas- Texas, Marekani sasa ni zamu ya watu wetu Navy Kenzo kuiwakilishakwenye headlines za tuzo za muziki Africa.
Kundi la muziki kutoka Bongo Flevani linaloundwa na wasanii wawili, Nahreel na Aika‘Navy Kenzo’ limechaguliwa kuwania Tuzo za muziki za Nigeria zinazoitwa Top Naija Music Awards 2015 zitakazofanyika tarehe 2 January 2016.

Hit Single ya Navy Kenzo ‘Game’ iliyotengenezwa South Africa na kusimamiwa naDirector Justin Campos wa Gorrila Films, South Africa imeweza kufanya vizuri sana na kupenya kwenye countdown mbalimbali za Radio na Tv Africa ikiwemo chati za Trace African Charts (TraceUrban), Sound City na hata chati ya MTV Base Official African Chart.
Makundi mengine ambayo Navy Kenzo watachuana nayo ni pamoja na Dupi 2, Connect Music Group (Cmg), Ace Republic, Dp-Kings na Betrose… na kupitia page yao yaInstagram, Navy Kenzo wamepost picha na link itakayokuwezesha kuwapigia kura moja kwa moja…
>>> “ Kundi
bora la muziki toka #+225 Navy Kenzo la chaguliwa kuwania kipengele cha
#KundiBoraLaMziki katika tuzo za #TopNaijaMusicAwards za nchini
nigeria..uwanja wa kupiga kura umeshafunguliwa kura yako ni muhimu sana
kwetu tunaomba ushirikiano wako.LINK YA KUPIGIA KURA IPO KWA BIO YETU... #AboveInAMinute #GameGame #ThankYouGuys
#VoteVoteVoteForUs” <<< @navykenzoofficial.

Milango ya kupiga kura imeshafunguliwa mtu wangu na ukitembelea hii link >>>topnaijamusicawards.com/vote/bestmusicgroup/ itakupeleka moja kwa moja kuwapigia kura Navy Kenzo kwenye kipegele cha Kundi bora la muziki (Best Music Group 2015).
Utaruhusiwa kuwapigia kura Navy Kenzo mara moja tu kwa siku na mwisho wa kupiga kura ni tarehe 31 December 2015.
Hapa chini nimekusogezea fomu ya kupiga kura utakayokutana nayo, ukifika hapo utachagua kundi la pili kwenye orodha ambalo ni Navy Kenzo.
No comments:
Post a Comment