
Ni staa wa bongofleva ambae hits
zilizompa headlines ni pamoja na ‘Tabasamu‘ aliyoshirikishwa na Mr.
Blue, msanii huyo tangu afunge ndoa October 11 2014 amekuwa kimya
katika tasnia ya Bongo Fleva sasa hapa ameyajibu yote.
Akiongea na ripota wa millardayo.com msanii huyo alisema..’Ni
kitu cha kawaida kwani kuoa ni kama kutoka stage moja na kwenda
nyingine ila sio kama nimekuwa kimya sana bali kuna baadhi ya mashabiki
wangu wanakuwa wananiona kwenye muziki wa bendi na mpaka sasa nipo na
bendi iitwayo Ina Afrika Band kuna project nilikuwa nazunguka nao
iitwayo Mama Africa inafanyika nchi za nje kama Ulaya’- Steve RNB
‘Lakini sio kama ni kweli kwamba tangu
niingie kwenye ndoa basi ndio imenifanya ni stop lakini this time
mashabiki nimetenga muda wao kwaajili ya kufanya muziki wa Bongo Fleva
ukiachana na muziki ninaoufanya kwa sasa wa Bendi kwa hiyo soon mambo
yote yatakuwa mazuri’ – Steve Rnb
No comments:
Post a Comment