
Waziri
Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.
Aidha,
Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama
Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye
Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru
Kenyatta.
Ameeleza
pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa
uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya
ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la
nchi hizo.
No comments:
Post a Comment