Wiki moja iliyopita, Mtanzania Agnes Masogange
alikuwa topic kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya post yake
kwenye Instagram kuzua mjadala na kuibua uvumi mkubwa sana kati yake na Davido staa wa muziki kutoka Nigeria… ambapo mitandao mingi ilidai kuwa Agnes ana ujauzito wa Davido! Je, taarifa hizi zina ukweli wowote?

Agnes Masogange.
Davido aliamua azungumze baada ya kuchoshwa na maneno yote yanyosemwa juu yake na Masogange kwenye tweets zake nane nilizofanikiwa kuzinasa kupitia page yake ya Twitter @iam_Davido.

Davido.
Haya ndio majibu ya Davido kuhusu uvumi wa Agnes Masogange kubeba ujauzito wake..

>>> “TBH sijali Blogs zinaandika nini Ukweli au Uongo lakini pale ambapo mtu ananipigia kutoka nchini nyingine analia… ” <<< @iam_Davido.

>>> “Kuhusu mchumba wake kuona taarifa za uongo na anakaribia kuondoka na kumuacha…” <<< @iam_Davido.

>>> “na
machungu!! Haya ni maisha ya watu ambayo nyie watu mnayachezea, mpaka
kitu cha ajabu kitokee ndipo watu watakapojiona wajinga…” <<< @iam_Davido.

>>> “Tafadhali acheni, hii sio haki kwa Agnes na mpenzi wake, waache waishi na kupata mtoto wao kwa amani… Smh” <<< @iam_Davido.

>>> “Nimetajwa kama miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa kwa mwaka 2015 na FORBES AFRICA kwanini msiisambaze hii” <<< @iam_Davido.

>>> “Lakini
taarifa yoyote mbaya mtaishambulia na kuiandika! Msinichukulie vibaya,
kama ni taarifa za ukweli basi hakuna ubaya wowote… ” <<< @iam_Davido.

>>> “Lakini kwanini msambaze uongo!!! Tunaishi kwenye dunia iliyovurugwa!! Hii social media tunaitumia kwa level nyingine” <<< @iam_Davido.

>>> “Siku moja mtakuja kuandika ujinga kuhusu mtu ambaye haiwezi hii presha na mtaona kitakachotokea!!!” <<< @iam_Davido.
No comments:
Post a Comment