Kikosi cha TP Mazembe ambacho kinaundwa na
watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kimeenguliwa kwenye
michuano ya FIFA Club World Cup inayoendelea kuchanja mbuga nchini
Japan baada kukubali kipigo cha magoli 3-0 mbele ya wenyeji Sanfrecce
Hiroshima kwenye mchezo uliomalizika kwenye dimba la Osaka Nagai
Stadium, Japan.
Wachezaji wa Sanfrecce Hiroshima pamoja na wa TP Mazembe wakiingia uwanjani tarari kwa mechi
Timu zote zilianza mchezo kwa kasi tangu kupulizwa filimbi ya kwanza.
Lakini Sanfrecce walianza kufumania nyavu za mazembe dakika ya 44
kipindi cha kwanza kupitia kwa Shiotani baada ya Yusuke Chajima kupiga
mpira wa kona uliotua kichwani kwa Sho Sasaki kisha kumkuta Shiotani
aliyefunga kwa shuti la karibu. Thomas Ulimwegu wa TP Mazembe akiachia shuti
Kikosi cha Mazembe kilizinduka na kuanza kutafuta goli la kusawazisha
ambapo Assale alionekana kuwa mwiba kwa upande wa Sanfrecce ambapo
alimjaribu golikipa wa Takuyo Hayashi mara mbili kwa mashauti ya mbali
bila mafanikio. Richard Boateng waTP Mazembe na Douglas wa Sanfrecce Hiroshima wakiwania mpira
Thomas Ulimwengu aliingia kipindi cha pili na ilibaki kidogo afunge
goli muda mfupi baada ya kuingia baada ya kukimbia na mpira kwa kasi
takribani mita 40 na kuachia shuti kali ambalo lilitoka centimeter
chache nje ya goli. Alipiga pia mpira wa adhabu ndogo ambao haukuzaa
matunda wakati mabingwa hao wa bara la Afrika wakiwa kwenye harakati za
kusaka goli la kusawazisha
Dakika ya 56 Kazuhiko Chiba alifunga bao la pili akiunganisha mpira
wa kona uliopigwa na Chajima na kuzidi kuwaweka Mazembe kwenye wakati
mgumu. Salif Coulibaly wa TP Mazembe akimkabili Douglas wa Sanfrecce Hiroshima
Asano alizima kabisa ndoto za waafrika za kusonga mbele kwenye
michuano hiyo baada ya kufunga bao la tatu na kuwaacha vijana na tajiri
Moise Katumbi wakiwa vichwa chini wasiamini kilichowakuta.
Matokeo hayo yameipa Sanfrecce Hiroshima tiketi ya kufuzu kucheza
nusu fainali ya mashindano ya FIFA Club World Cup ambapo watakutana na
River Plate kwenye mchezo huo wa nusu fainali. Kazuhiko Chiba wa Sanfrecce Hiroshima akishangilia baada ya kufunga goli
No comments:
Post a Comment